Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Waziri Mkuu

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya

( DCEA )

SOBER HOUSES

Nyumba za upataji nafuu ni nini?

Ni Sehemu ambayo huwasaidia waraibu ambao bado wako kwenye matumizi ya vilevi kuachana navyo au kupata nafuu kwa kutumia hatua 12 za upataji nafuu pamoja na unasihi.

Huduma katika nyumba za upataji nafuu huendeshwa na asasi za kiraia ambapo waraibu wa dawa za kulevya wanapata huduma kwakupitishwa kwenye hatua hizo bila kutumia dawa ya aina yoyote. Matibabu haya hutolewa kwa malipo kwa waraibu wa dawa zote za kulevya kwa muda usiopungua miezi minne.

Serikali inaratibu uanzishwaji na kusimamia uendeshwaji wa Nyumba za Upataji Nafuu kwa kutumia Mwongozo wa Uanzishaji na Uendeshaji wa Nyumba za Upataji NafuuTanzania Bara. Hadi kufikia mwezi Februari 2022, kulikuwa na jumla ya nyumba 45 zinazotoa huduma hiyo katika mikoa ya Kilimanjaro, Tanga, Dares Salaam,Pwani, Dodoma, Morogoro, Iringa, Mwanza, Kagera, Tabora na Arusha.

Katika huduma hii watumiaji wa dawa za kulevya husaidiana wenyewe kwa wenyewe ambapo waraibu waliopata nafuu (kuacha matumizi ya dawa hizo kwa kipindi kisichopungua mwaka mmoja) huwaongoza waraibu wanaojiunga kushiriki mikutano ya Ustiri wa Mihadarati, (Narcotic

Anonymous) ambapo hupitishwa kwenye hatua kumi na mbili za upataji nafuu pamoja na unasihi. Waraibu wanaojiunga huweza hupatiwa mafunzo ya ujasiriamali, kazi za mikono pamoja na kushiriki katika shughuli za michezo.

Click here to view the list of recovery houses in Tanzania