(DCEA)
Bangi ni aina ya Dawa ya Kulevya inayotokana na Mmea uitwao Cannabis Sativoe. Majani ya Bangi yana Kemikali nyingi zinazoweza kuleta madhara katika mwili wa binadamu. Moja ya Kemikali ambayo imefanyiwa utafiti sana ni Tetrahydrocanabinoid(THC).
Matumizi ya Bangi husababisha utegemezi pamoja na madhara mengine ya kimwili na kiakili. Mbegu za Bangi hazina kiwango kikubwa cha THC hivyo matumizi ya Mbegu za Bangi kama kiungo cha mboga hayana madhara makubwa ya kiafya kulinganisha na uvutaji na majani.
Hata hivyo inashauriwa kuwa ikiwezekana watu watumie aina nyingine za viungo badala ya kutumia Mbegu za Bangi.
Dawa za kulevya zinazokamatwa hutunzwa kwenye Ghala maalum la kutunzia Vielelezo vya Kesi. Dawa hizi zinatakiwa kuwepo muda wote wa Kesi kama Kielelezo cha Kesi husika.
Pale Kesi zinapomalizika, Dawa hizi huteketezwa kwa taratibu zilizowekwa Kisheria. Tarehe 8 mwezi Oktoba .mwaka 2019 kiasi cha kilo 192 za Dawa za Kulevya aina ya Cocainei na Heroin zilichomwa katika Tanuru la kiwanda cha Cement Twiga kilichopo Wazo Hill baada ya Kesi zake kuisha.
Methadone ni Dawa inayotumika kutibu watu walioathirika na Matumizi ya Dawa za Kulevya aina ya Heroin ili kuzuia Arosto wanayoweza kupata pindi wanapokosa Dawa ya Heroin.
Dawa hii hotolewa Hospitalini kwa maelezo ya Daktari. Iwapo mtu ataitumia kiholela inaweza kumletea madhara na hata kifo.
Methadone haiwezi kutumika kama Dawa ya Kulevya kwani haileti raha baada ya kuitumia kama ilivyo kwenye Dawa zingine za Kulevya.
Kuberi na Ugoro ni bidhaa zinazotumiwa na watu wengi kwa ajili ya kujistarehesha. Bidhaa hizi ni aina ya vilevi visivyo dhibitiwa Kisheria. Kuber na ugoro zina viwango vya kemikali iitwayo Nicotine.
Mtu akitumia ugoro na kuberi huweza kumsababishia madhara kama;-
- Utegemezi,
- Saratani ya Mdomo, Fidhi na Koo na
- Mdomo kutoa harufu mbaya.
Kutokana na madhara hayo watu wanashauriwa kuachana na Matumizi ya Ugoro na Kuberi.
Majani ya Chamkwale hutumiwa mkoani Kigoma kama kilevi, Je yapo kwenye orodha ya dawa za kulevya?
Kinywaji cha Cocacola ni kinywaji kinachotumika dunia nzima. Kinywaji hiki kilianza kutengenezwa rasmi mwaka 1886. Kipindi hicho kinywaji hiki kilikuwa kinachanganywa na majani ya Coca yanayotummika kutengeneza Cocaine.
Kutokana na hali hiyo kulitokea malalamiko makubwa kutoka kwa jamii juu ya kuchanganya Cocaine kwenye Cocacola. Mwaka 1093 watengenezaji wa Cocacolawalipunguza kiasi kikubwa cha Cocaine kwenye kinywaji cha cocacola. Mwaka 1929 wanasayansi walifanikiwa kuondoa kabisa kiambata cha Cocaine katika cocacola.
Hivyo basi, kinywaji cha Cocacola kinachotumika sasa hivi hakina Cocaine.
Kutokana na kemikali hizo katika mirungi, watumiaji wa mirungi wamekuwa wakipata madhara mbalimbali ya kimwili na kiakili. Baadhi ya madhara hayo ni;
Huongeza kasi ya mapigo ya moyo hivyo kuweza kuongeza shinikizo la damu, kiharusi na hata kusababisha kifo.
Husababisha vidonda vya utumbo mdogo, saratani ya mdomo, koo na tumbo
Husababisha upungufu wa msukumo wa kufanya tendo la ndoa, kumaliza haraka na kutoweza kudumu kwenye tendo la ndoa kwa muda mrefu
Hupunguza ubora wa mbegu za kiume na kuvuruga mfumo wa utokaji wake na hata kusababisha ugumba
Mtumiaji hukosa usingizi na ulevi ukiisha mwilini husababisha usingizi mzito unaoweza kusababisha ajali hasa kwa madereva
Huchochea ukatili, fujo, ugomvi, kuongea sana masuala ya kusadikika na kuhangaika.
Mtumiaji hukosa kabisa hamu ya kula na kupungua uzito.
Mirungi husababisha upungufu wa maji mwilini na kuleta tatizo la kukosa choo pamoja na ugonjwa wa bawasiri
Mtumiaji mirungi akiikosa mirungi hupata uchovu, sonona, hasira za ghafla, kutetemeka, kushindwa kutulia na njozi za kutisha (night mares)
Utumiaji mirungi huozesha meno na yale yanayosalia hubadilika rangi, fizi kuuma na harufu ya mdomo.
Mirungi huharibu ufanisi wa ini mwilini katika kuchuja sumu za mwili
Mirungi huamsha magonjwa ya akili yanayojitokeza kwa vipindi “mwezi mchanga” kwa watumiaji wenye tatizo hilo
Matumizi ya mirungi wakati wa ujauzito yanaweza kusababisha kuzaliwa kwa watoto wenye uzito mdogo ambao huweza kukataa kunyonya kutokana na ladha ya maziwa kubadilishwa na viuatilifu vinavyotumika kwenye kilimo cha mirungi.
Kutokana na madhara hayo, kongamano la Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kupiga vita dawa za Kulevya na uhalifu (UNODC) la mwaka 1971 liliamua kuorodhesha Mirungi kuwa miongoni mwa dawa za kulevyana kupiga marufuku utafunaji wa mirungi. Kwa kuwa Tanzania ni Mwanachama wa umoja wa mataifa na tunaunga mkono kongamano hilo, tunawajibika kupiga marufuku matumizi ya mirungi.
Kitendo cha nchi nyingine kuhalalisha matuikzi ya mirungi siyo sababu ya kutufanya na sisi tuhalalishe. Kuna baadhi ya nchi zimehalalisha ndoa za jinsia moja, je na sisi tuige? Baadhi ya nchi za Ulaya ambazo awali ziiruhusu matumizi ya mirungi zimeanza kuiharamisha baada ya kuona madhara yake.
Dawa gani zinatumiwa sana?
Nitamjiuaje mtumiaji
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya
S.L.P 80327
8 Barabara ya Kivukoni Front, 11486 Dar es salaam
Dar es Salaam
Simu: +255 22 211 3754/57
Nukushi: +255 22 211 3752
Barua pepe: cg@dcea.go.tz
© 2023 Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya. Haki zote zimehifadhiwa..
Imesanifiwa, Imetengenezwa, na Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) na Inaendeshwa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya