Ushirikishwaji wa sekta binafsi katika udhibiti wa kemikali bashirifu
Ushirikishwaji wa sekta binafsi katika udhibiti wa kemikali bashirifu
Chini ya udhamini wa Bodi ya Kimataifa ya Kudhibti dawa za kulevya INCB, Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za kulevya (DCEA) kwa kushirikiana na mamlakanyingineza udhibiti za TMDA, GCLA, MSD na Baraza la Famasi nchini zinatekeleza mradi wa kushirikisha sekta binafsi kuzuia uchepushwaji wa kemikali bashirifu.
Ushirikishaji huo ni muhimu katika kufanikisha utekelezaji wa Sheria za udhibiti kikamilifu kwani wadau muhimu wanakuwa sehemu ya udhibiti na hivyo kuziwezesha mamlaka kupata taarifa za uchepushwaji kwa wakati.