Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Waziri Mkuu

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya

( DCEA )

Misingi Muhimu

  • Uadilifu

Kuzingatia kanuni za uadilifu na ukweli ili kutenda haki bila upendeleo.

  • Ushirikiano

Kuimarisha ushirikiano na wadau pamoja na jumuiya ya kimataifa katika jitihada za kupambana na kudhibiti dawa za kulevya.

  • Uwajibikaji

Kufanya kazi kwa kuzingatia maslahi ya umma ili kuilinda jamii dhidi ya matumizi, biashara na madhara ya dawa za kulevya.

  • Ubunifu

Matumizi ya njia/mbinu bora zaidi zinazokidhi kutatua changamoto mpya katika udhibiti wa dawa za kulevya.

  • Weledi

Kuwa na timu ya wataalamu wanaofanya kazi kwa weledi na maarifa.

  • Usiri

Kuweka siri ya vyanzo vya taarifa za dawa za kulevya ili kuwalinda watoa taarifa.

  • Ufanisi

Kufanya kazi kwa bidii na maarifa ili kutimiza malengo.