Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Waziri Mkuu

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana Dawa za Kulevya

( DCEA )

Huduma za matibabu kwa waathirika wa dawa za kulevya

Kuna aina mbalimbali za matibabu kwa waraibu wa dawa za kulevya ingawa hakuna tiba moja ambayo inafaa kwa waraibu wote. Matibabu ya uraibu wa dawa za kulevya hutofautiana sana kulingana na aina ya dawa husika, kiasi cha dawa kilichotumika, muda wa uraibu, matatizo ya kiafya na mahitaji ya kijamii na mtu binafsi.

Huduma za tiba ya uraibu zinazotolewa nchini ni:

  1. Tiba saidizi kwa waraibu kwa kutumia dawa (Medically Assisted Therapy - MAT)
  2. Huduma katika Nyumba za Upataji Nafuu (Sober Houses)
  3. Tiba kwenye vituo vya kutolea Huduma za Afya ya Akili.

Hata hivyo, kuna baadhi ya waraibu wanaopatiwa huduma za unasihi pekee kwenye asasi za kiraia na kuachana na matumizi ya dawa hizo.