Dawa mpya za kulevya
Dawa mpya za kulevya
Dawa mpya za kulevya ni dawa za kulevya ambazo hutengenezwa katika maabara bubu (clan laboratories) na haziko kwenye udhibiti chini ya mikataba ya kitaifa na kimataifa.
Dawa mpya za kulevya zinaweza kusababisha madhara makubwa kwa afya ya mtumiaji, zinafahamika kama dawa za kulevya zikiwa zenyewe au katika mchanganyiko na dawa nyinginezo.
Dawa hizi ambazo hazidhibitiwi kimataifa, hutengenezwa makusudi kukwepa mifumo ya udhibiti wa dawa za kulevya zilizopo kwenye orodha ya dawa zinazodhibitiwa. Dawa hizi zipo kwenye makundi mbalimbali kama vile cannabinoids, phenethylamines, synthetic cathinones, tryptamines, fentanyl related substances etc