Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Waziri Mkuu

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana Dawa za Kulevya

( DCEA )

Medication Assisted Therapy Clinics (MAT CLINICS)

VITUO VYA TIBA SAIDIZI KWA WARAIBU KWA KUTUMIA DAWA (MEDICALLY ASSISTED THERAPY - MAT)

Vituo hivi husimamiwa na serikali na huhudumia waathirika wa dawa ya kulevya aina ya afyuni kama vile heroin na baadhi ya dawa tiba zenye asili ya kulevya. Waathirika wanaotibiwa kwenye vituo hivi hutibiwa kwa kutumia dawa mfano Methadone. Waathirika wanatakiwa kuhudhuria matibabu kila siku mpaka watakapomaliza matibabu. Huduma ya MAT hutolewa bure chini ya uangalizi wa wataalamu.

HUDUMA ZINAZOTOLEWA KATIKA VITUO VYA TIBA SAIDIZI KWA WARAIBU KWA KUTUMIA DAWA (MAT)

1.Kupatiwa dawa aina ya methadone
2.Kupatiwa Elimu juu ya UKIMWI na Kupima VVU
3.Kupatiwa dawa za kufubaza VVU (Antiretroviral therapy)
4.Kupatiwa elimu ya Kinga, Kupima na kutoa matibabu kwa wagonjwa wa Kifua kikuu.
5.Kupatiwa elimu ya Kinga na kutibu Magonjwa ya zinaa
6.Kupatiwa Ushauri nasaha
7.Kupatiwa matibabu ya magonjwa ya Akili
8.Kupatiwa Elimu juu ya maambukizi ya Homa ya ini B na C


ORODHA YA VITUO VYA METHADONE NA MAHALI VILIPO

Na

JINA LA KITUO

JINA LA HOSPITALI

MKOA

1.

Kliniki ya MAT Muhimbili

Hospitali ya Taifa Muhimbili

Dar es Salaam

2.

Kliniki ya MAT Mwananyamala

Hospitali ya Mkoa ya Rufaa Mwananyamala

Dar es Salaam

3.

Kliniki ya MAT Temeke

Hospitali ya Mkoa ya Rufaa Temeke

Dar es Salaam

4.

Kliniki ya MAT Mbeya

Hospitali ya Rufaa ya Kanda

Mbeya

5.

Kliniki ya MAT Mwanza

Hospitali ya Mkoa ya Rufaa ya Sekou Toure

Mwanza

6.

Kliniki ya MAT Itega

Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe

Dodoma

7.

Kliniki ya MAT Bagamoyo

Hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo

Pwani

8.

Kliniki ya MAT Tanga

Hospitali ya Mkoa ya Rufaa ya Bombo

Tanga

9.

Kliniki ya MAT Tumbi

Hospitali ya Rufaa yaMkoa ya Tumbi, Kibaha

Pwani

10.

Kliniki ya MAT Arusha

Hospitali ya Mkoa ya Rufaa yaMkoa, Mount Meru- Arusha

Arusha

11.

Kliniki ya MAT Tunduma

Kituo cha Afya cha Tunduma

Songwe

12.

Kliniki ya MAT Segerea

Kituo cha Afya cha Segerea

Dar es Salaam

13.

Kliniki ya MAT Tegeta

Kituo cha Afya cha Tegeta

Dar es Salaam

14.

Kliniki ya MAT Mbagala

Zahanati ya Round Table-Mbagala

Dar es Salaam

15.

Kliniki ya MAT Kigamboni

Hospitali ya Vijibweni-Kigamboni

Dar es Salaam

JINSI YA KUJIUNGA NA VITUO HIVYO

 • Ili uweze kujiunga na vituo hivi, lazima upitie kwenye asasi za Kiraia CSOs zilizo kasimiwa kupeleka waraibu katika vituo hivyo vya Methadone.
 • Waraibu watapatiwa elimu juu ya matibabu ya methadone na baadaye kuunganishwa na jamaa zao ili waweze kuwasaidia.
 • Mafunzo huchukua takribani majuma mawili
 • Baada ya mafunzo, Waraibu watapelekwa kwenye vituo vya Methadone kuanza dawa.
 • Jamaa zao watatakiwa kuwasaidia waraibu kwa kuwapatia nauli ya kuhudhuria matibabu, chakula na malazi. Hatua hii inasaidia katika uponaji wa muraibu.

NINI FAIDA YA TIBA YA METHADONE

 • Inaondoa utegemezi wa dawa za kulevya aina ya heroin
 • Inapunguza hatari ya mtegemezi kuwa katika hali ya kupata maambukizi ya HIV, homa ya ini na kifua kikuu.
 • Inaimarisha mwili na kumfanya mgonjwa kurudi katika hali yake ya kawaida
 • Inaboresha mfumo wa mwili na kupunguza hatari za matumizi yasiyo sahihi ya dawa kwa kuzidisha kiwango
 • Kuimarisha mfumo wa uzazi
 • Kupunguza vifo vya ghafla vitokanavyo na matumizi mabaya ya dawa za kulevya.
 • Inasaidia kupunguza mzunguko wa pesa chafu kwa wauzaji na wasambazaji
 • Huleta mabadiliko chanya ya tabiana kupunguza vitendo vya kihalifu na uvunjaji wa amani
BAADHI YA CSOs ZINAZOPELEKA WARAIBU KATIKA VITUO VYA METHADONE

MEFADA

GIFT OF HOPE FOUNDATION