Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Waziri Mkuu

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana Dawa za Kulevya

( DCEA )

Tanzania yaendelea kushirikiana na Mataifa Duniani katika kupambana na dawa za kulevya

Imewekwa: 22 October, 2021
Tanzania yaendelea kushirikiana na Mataifa Duniani katika kupambana na dawa za kulevya

Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Gerald Musabila Kusaya, akiambatana na ujumbe mwingine wa Mamlaka ameiwakilisha Tanzania katika mkutano wa 64 wa majadiliano ya kamisheni ya kimataifa ya udhibiti wa dawa za kulevya duniani ulioanza Oktoba 19 – 21 mwaka huu jijini Vienna Nchini Austria.

Mkutano huo una lengo la kujadili makubaliano ya utekelezaji wa sera ya dawa za kulevya kimataifa, kuimarisha ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa pamoja na kutatua changamoto zinazojitokeza katika mapambano dhidi ya tatizo la dawa za kulevya.

Pia, mkutano huo umejadili namna bora ya kupambana na tatizo la dawa za kulevya na makosa mengine ya uhalifu wa kupangwa ikiwemo ugaidi, utakatishajifedha, usafirishaji haramu wa binadamu, uharifu wa kimtandao, kuimarisha ushirikiano wa kikanda na kimataifa pamoja pamoja na kutatua changamoto zinazojitokeza katika mapambano ya dawa za kulevya duniani.


fWajumbe wa mkutano kutoka mataifa mbalimbali wakiendelea na mkutano


fkamisha jenerali Kusaya (Kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na mwenyekiti wa mkutano huo Balozi Dominika Krois (kushoto) na Jo -Dedeyne - Amann ambae ni katibu mtendaji.


Mwisho