Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Waziri Mkuu

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana Dawa za Kulevya

( DCEA )

Picha za Matukio - NBAA Awards

Imewekwa: 18 December, 2019
Picha za Matukio - NBAA Awards

Tarehe 7 Disemba mwaka huu, Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) ilishinda na kukabidhiwa Tuzo ya mshindi wa kwanza ya umahiri katika utayarishaji bora wa taarifa za hesabu kwa mwaka 2017/2018 kwa kufuata viwango vya Kimataifa vya Uandaaji wa Hesabu (International Public Sectors Accounting Standards - IPSAS) katika kundi la Wizara, Idara na Taasisi za Serikali. Zifuatazo ni picha za baadhi ya matukio katika ugawaji wa tuzo


H

Kamishna msaidizi wa Huduma za Taasisi wa Mamlaka Bi. Doroth Buchanagandi akipokea tuzo baada ya kutangazwa washindi.


H

Kamishna msaidizi wa Huduma za Taasisi wa Mamlaka Bi. Doroth Buchanagandi akionesha tuzo kwa waalikwa baada ya kukabidhiwa.



J

Timu ya wahasibu wa Mamlaka katika picha ya pamoja na Kamishna msaidizi wa Huduma za Taasisi. Kutoka Kulia kushoto ni muhasibu mkuu CPA Lupakisyo Mwakitalima, aliyeshika tuzo ni muhasibu mwandamizi Bw. Mtaki Eusechu akifuatiwa na Muhasibu Morris A. Kisara.


JMwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya wahasibu na wakaguzi wa hesabu Prof. Isaya Jairo akimkaribisha mgeni rasmi ambae ni naibu katibu mkuu wa Wizara ya fedha na Mipango.

Y

Kamishna, na tibmu ya wahasibu wa Mamlaka wakiungana na waalikwa wengine kumkaribisha mgeni rasmi alipokuwa akiwasili ukumbini.


I

Wawakilishi wa Mamlaka wakigonga glass na waalikwa wengine kama ishara ya kufuurahia ushindi katika hafla ya ugawaji tuzo.


I

Washindi wa kwanza kutoka sehemu mbalimbali katika picha ya pamoja na mgeni rasmi.


hPicha ya muhasibu mkuu wa Mamlaka akiwa na tuzo.

7Picha ya muhasibu mwandamizi wa Mamlaka akiwa na tuzo.

U