Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Waziri Mkuu

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana Dawa za Kulevya

( DCEA )

DCEA yaendelea kung`ara tuzo za NBAA

Imewekwa: 13 December, 2019
DCEA yaendelea kung`ara tuzo za NBAA

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imeshika nafasi ya kwanza na kunyakua tuzo ya umahiri katika utayarishaji bora wa taarifa za hesabu kwa mwaka 2017/2018 kwa kufuata viwango vya Kimataifa vya Uandaaji wa Hesabu International Public Sectors Accounting Standards (IPSAS) katika kundi la Wizara, Idara na Taasisi za Serikali.

Tuzo hiyo imetolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi (NBAA) katika hafla iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha NBAA APC hotel Bunju jijini Dar es Salaam. Hii ni mara ya tano kwa Mamlaka kushiriki katika mashindano hayo na kuwa mshindi kama ifuatavyo; - mwaka 2015 ilishika nafasi ya kwanza, mwaka 2016 ilishika nafasi ya tatu, mwaka 2018 nafasi ya kwanza, na mwaka 2019 nafasi ya kwanza. Mamlaka imenyakua tuzo ya mshindi wa kwanza kwa mara pili mfululizo.

Kutokana na mafanikio ya tuzo hiyo, kaimu kamishna jenerali wa Mamlaka Bw. James Kaji amekipongeza Kitengo cha fedha na uhasibu na idara nyingine ndani ya mamlaka kwa kufanikisha uandaaji bora wa hesabu uliopelekea kuwa washindi wa tuzo hiyo.

“Uandaaji bora wa taarifa za hesabu ni moja ya ufanisi wa ofisi yoyote hivyo nawapongeza sana Kitengo cha fedha na Uhasibu pamoja na idara nyingine kwa kutoa mchango mkubwa kuhakikisha Kitengo cha fedha na uhasibu kinafanya vizuri” amesema kamishna Kaji.

Nae muhasibu mkuu wa Mamlaka CPA. Lupakisyo Mwakitalima amesema ushindi huu umetokana na ushirikiano wa divisheni, vitengo, na sehemu zote za Mamlaka. Hivyo amewaomba watumishi kuendelea kuchapa kazi ili Mamlaka iendelee kung’ara.

Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi (NBAA)) hutoa tuzo hizi kila mwaka kwa kushindanisha wizara, taasisi, mashirika, na kampuni mbalimbali nchi nzima.

h

Baadhiya washindi wa tuzo katika picha ya pamoja. Wa pili kutoka kushoto nyuma ni CPA Mwakitalima akifuatiwa na Kaimu kamishna wa Huduma za Taasisi wa Mamlaka Bi. Doroth Buchanagandi.