Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Waziri Mkuu

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana Dawa za Kulevya

( DCEA )
Nilinusurika kufa kwa kusafirisha dawa za kulevya
Nilinusurika kufa kwa kusafirisha dawa za kulevya

Kwa jina naitwa Jimmy Batistuta natokea Dar es Salaam. Niko katika Sober House ya Kigamboni. Mimi nilipata madhara makubwa kutokana na Dawa za Kulevya. Nimefanyiwa upasuaji mkubwa mara mbili kutokana na usafirishaji wa Dawa za Kulevya.

Mara ya kwanza nilikamatwa Islamberg nikawekwa chini ya ulinzi na kwenda kupasuliwa, mara ya pili nilijipeleka Muhimbili hospitali mimi mwenyewe kutokana na upasuaji wa awali kuniletea matatizo . baada ya upasuaji wa kwanza niliendeea kutumia dawa za kulevya na kitaalamu kidonda cha dawa za kulevya hakiponi kama mgonjwa anaendelea na matumizi. Kwahiyo nilitembea na kidonda kwa miaka 6 kwenda saba kikiwa kinavuja usaha na damu muda wote.

Ninamshukuru Mungu nilipata msaada na kuacha kabisa matumizi ya Dawa hizo na sasa ni mzima. Nataka niwaase vijana wenzangu maana vijana wengi tunatumika kutokana na urubuni wa pesa. Tukumbuke kuna kufungwa, kunyongwa na hata kufa.

Nawapongeza Mamlaka kwa udhibiti walioufanya. Nawashukuru madaktari kwa kuokoa maisha yangu pale Muhimbili. Nawashukuru viongozi wote wa jiji la Tanga . Tanzania bila dawa za kulevya inawezekana