Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Waziri Mkuu

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya

( DCEA )
Dawa za kulevya zilivyoharibu ndoto zangu
Dawa za kulevya zilivyoharibu ndoto zangu

Naitwa Jackline Peter Mfughala. nimetumia dawa za kulevya kwa muda wa miaka mitano. Nilianza kujiingiza kwenye matumizi ya dawa za kulevya nilipomaliza kidato cha nne, wakati niko “idle” nyumbani nikisubiri majibu ya mitihani. Nilijikuta nimeingia kwenye makundi mabovu yaliyonipelekea kuwa mtumiaji na hatimaye mtegemezi wa dawa za kulevya. Nimepitia changamoto nyingi sana nikiwa binti mdogo.

Matokeo ya kidato cha nne yalipotoka nilifaulu vizuri sana ila sikuweza kuendelea na kidato cha tano na cha sita kwa sababunilikuwa nimeshakuwa mtegemezi wa dawa za kulevya.

Matumaini yangu yalirejea baada ya kujiunga na huduma na tiba ya methadone ambapo niliweza kupata mafunzo ya darasani na dawa ya methadone iliyonisaidia kupona.Namshukuru Mungu niliweza kurejea kuendelea na masomo yangu ya kidato cha tano na cha sita. Pia nashukuru kwa mafunzo niliyoyapata nilipokuwa kwenye tiba kwani mafunzo hayo yamenisaidia kuanzisha asasi yangu ambayo inatoa elimu kwa vijana wa kike kuhusiana na athari za dawa za kulevya.

Naishukuru Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, nawashukuru wauguzi wote wanaosaidia kufanikisha tiba kwa waraibu wa dawa za kulevya, nawashukuru MDH, naishukuru Serikali kwa kutoa huduma ya methadone bure, pia nawashukuru wanaharakati wote wanaopambana na dawa za kulevya.

Nitoe wito wa vijana wenzangu madawa kuachana na matumizi ya dawa za kulevya kwani yanakatisha ndoto na kupoteza mwelekeo, unaweza kuanza kama starehe lakini baadae inakuwa majuto. Hivyo nawashauri kutokujiingiza kabisa kwenye dawa za kulevya.


Tanzania bila dawa za kulevya inawezekana