Methodone imenijereshea utu wangu
Kwa jina naitwa Baraka Moses Shangwi natokea mwananyamala Dar es Salaam. Kwa kifupi kabisa mimi nimekuwa nikitumia madawa kwa zaidi ya miaka 10. Matumizi hayo yalipelekea mimi kupoteza ajira. Awali nilikuwa nimeajiriwa kama mwalimu hivyo kutokana na matumizi ya Dawa za Kulevya nilipoteza ufanisi na sikuweza kufanya kazi tena.Kwahiyo kazi ikafa na majanga yakaanza. Kazi ilipokufa nikajitafakari nikaona niende chuo, na chuo kikafa nikiwa mwaka wa pili kutokana na sababu hizo hizo za kushindwa kumudu masomo. Wazazi wangu hawakupenda kitendo changU cha kutumia Dawa hivyo uaminifu kwa familia ukafa na nikatengwa, marafiki wakaniacha maana hatukuwa level moja tena. Rafiki yangu aligeuka kuwa unga na adui yangu mkubwa akawa arosto.
Ilifika kipindi nikakata tamaa kabisa. Bahati nzuri nikakutana na Methadone na nikaanza tiba. Kwa hali niliyokuwa nimefikia bila methadone nisingekuwa hai. Nilianza kupata matibabu na ushauri na baada ya muda fulani mambo yakaanza kujirekebisha na afya ikaanza kurudi, utambuzi pia ukaanza kurudi, taratibu nikaanza kuwa binadamu kama nilivyolelewa na wazazi wangu.
Tiba ya methadone imenisaidia kuacha kabisa matumizi ya Dawa za Kulevya na kuniondolea uraibu niliokuwa nao. Pili imenirejeshea afya, na tatu imenirejeshea uaminifu nilioupoteza kwa watu. Japo uaminifu haujarudi kwa watu wote ila kwa kiasi flani nimeanza kuaminika tena.
Nimefanya kazi na taasisi mbalimbali kama MDH, kupitia MDH tumevumbua asilimia 17 ya wagonjwa wa kifua kikuu kitaifa. Hii ni ushahidi wa wazi kuwa tunaweza. Tulikuwa binadamu madawa yakatutoa katika hali ya ubinadamu sasa tumerudi kuwa binadamu tena. Tunahitaji msaada wa kuweza kufanikisha malengo tuliyoyapoteza kwa miaka mingi.
Nawashukuru Madaktari wengi waliotuhudumia. Bila kumsahau raisMagufulikwa kutukombea vijana wake kupitia Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana naa Dawa za Kulevya. Mapapa wamekamatwa hakuna unga mtaani, watu wana haha huko mitaani, nawashauri waache kuhaha badala yake waende vituo vya tiba kupata tiba. Pia naishauri serikalikufungua vituo vingi vya afya ili viweze kutusaidia.