Tani 9.93 za Dawa za Kulevya na Chupa 1,795 za Dawa Tiba Zenye Asili ya Kulevya Zakamatwa Nchini
Tani 9.93 za Dawa za Kulevya na Chupa 1,795 za Dawa Tiba Zenye Asili ya Kulevya Zakamatwa Nchini
04 March, 2026
Pakua
Mwezi Januari na Februari 2026, Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya imekamata tani 9.93 za dawa za kulevya aina mbalimbali, chupa 1,795 za dawa tiba zenye asili ya kulevya na kuteketeza ekari 87.5 za mashamba ya bangi. Magari 6 na pikipiki 29 vilikamatwa katika operesheni hizo huku watuhumiwa 151 wakikamatwa kuhusika na uhalifu huo.