Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Waziri Mkuu

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana Dawa za Kulevya

( DCEA )

DCEA yatoa mafunzo kwa waingizaji, wazalishaji na wasambazaji wa kemikali bashirifu na dawa tiba zenye asili ya kulevya

Imewekwa: 26 September, 2019
DCEA yatoa mafunzo kwa waingizaji, wazalishaji na wasambazaji wa kemikali bashirifu na dawa tiba zenye asili ya kulevya

Nchini Tanzania Kumekuwa na matukio mengi ya uchepushwaji wa kemikali bashirifu na matumizi mabaya ya dawa tiba zenye asili ya kulevya.Juhudi mbalimbali zimekuwa zikifanywa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) kwa kushirikiana na taasisi zinazohusika na udhibiti wa dawa na kemikali bashirifu.Hata hivyo taasisi hizi za serikali zimeona ni vema kuzishirikisha sekta binafsi katika kudhibiti tatizo hilo.

Katika kufanikisha azma hiyo, Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) kwa kushirikiana na TMDA, GCLA, MSD, na PC imeanza kutekeleza mradi wa ushirikishwaji wa sekta binafsi katika kudhibiti uchepushwaji wa kemikali bashirifu na dawa tiba zenye asili ya kulevya. Mwezi Septemba mwaka huu Mamlaka kwa kushirikiana na taasisi hizo imetoa mafunzo kwa waingizaji, wazalishaji na wasambazaji wa dawa hizo, lengo likiwa kuwajengea uelewa wa namna gani serikali na sekta binafsi zinaweza kushirikiana katika kudhibiti uchepushwaji wa dawa tiba zenye asili ya kulevya na kemikali bashirifu (Public Private Partnership in preventing diversion of precursors)

Mada zilizotolewa ni pamoja na uchepushwaji wa kemikali bashirifu na matumizi mabaya ya dawa tiba zenye asili ya kulevya unavyofanyika, sheria zinazohusika na udhibiti wa uchepushwaji pamoja na uanzishwaji wamradi wa ushirikiano kati ya serikali na sekta binafsi (PPP).

Wajumbe wakifatilia kikao

Akizungumza katika semina hiyo, afisa kutoka Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya ameyataja maeneo ambao uchepushwaji unaweza kufanyika kuwa ni wakati wa uzalishaji, uingizaji, usafirishaji na wakati wa uchakataji na hata wakati wa uteketezaji.

Utekelezaji wa mradi huu nchini umetokana na mafunzo yaliyotolewa na Taasisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na udhibiti wa dawa za kulevya (INCB) kwa maafisa wa taasisi zinazohusika na udhibiti wa uchepushwaji wa kemikali bashirifu na dawa tiba zenye asili ya kulevya.

Afisa kutoka DCEA akiwasilisha mada

mjumbe akichangia wakati wa uwasilishaji