Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Waziri Mkuu

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana Dawa za Kulevya

( DCEA )

Tiba

Imewekwa: 16 January, 2017
Tiba

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya inashirikiana  na wadau mbalimbali katika kupunguza madhara ya dawa za kulevya kwa kutoa tiba, huduma za utengamao na elimu ya upunguzaji madhara kwa waraibu wa dawa za kulevya. Jitihada hizo ni pamoja na kupanua na kuimarisha huduma za tiba katika vitengo mbalimbali vya afya ya akili, tiba saidizi kwa waraibu kwa kutumia dawa ( Medically Assisted Therapy -MAT), nyumba za upatajinafuu na huduma za unasihi.