KAMISHNA JENERALI KUSAYA ALIPOTEMBELEA MAMLAKA YA MAABARA YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI (GCLA)
KAMISHNA JENERALI KUSAYA ALIPOTEMBELEA MAMLAKA YA MAABARA YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI (GCLA)
Kamishna jenerali Kusaya akiambatana na makamisha wengine ameitembelea Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Makao Makuu kuweza kuona namna shughuli za uchunguzi wa kimaabara wa sampuli za dawa za kulevya unavyofanyika. Katika ziara hiyo Kamishna Jenerali Kusaya aliweza kutembelea Maabara ya Sayansi Jinai Kemia, Toksikolojia na Maabara ya Mitambo.