Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Waziri Mkuu

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya

( DCEA )

Waziri Lukuvi aipongeza DCEA

Imewekwa: 06 October, 2024
Waziri Lukuvi aipongeza DCEA

Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. William Lukuvi amewapongeza watumishi wa Mamlaka ya kudhibiti na Kupambana na dawa za kulevya (DCEA) kwa kazi  nzuri wanayoifanywa ya kupambana na tatizo la dawa za kulevya nchini.

Waziri Lukuvi ameyasema hayo wakati alipofanya ziara rasmi Septemba 25, 2024 katika ofisi za makao makuu ya Mamlaka hiyo, Hii ikiwa ni mara ya kwanza tangu Rais Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan kumteua na kushika wadhifa huo.  

Akizungumza na watumishi wa DCEA, Waziri Lukuvi amesisitiza umuhimu wa kazi wanayoifanya, akibainisha kuwa ingawa haina matokeo ya mfukoni, ina thawabu kubwa kutoka kwa Mungu kwa kuwa inaokoa maisha ya watu wengi. “Kazi yenu ni muhimu sana kwa usalama wa taifa letu na wananchi wake,” alisema Waziri Lukuvi.

Mhe. William Lukuvi akizungumza na watumishi wa DCEA kuhusu umuhimu wa kazi yao katika kuokoa maisha na kudhibiti tatizo la dawa za kulevya.

Waziri Lukuvi ameeleza kuwa juhudi za Serikali katika kupambana na dawa za kulevya zimeanza kuzaa matunda, na Tanzania sasa inajulikana kwa msimamo wake thabiti dhidi ya biashara hii haramu. “Tuna uwezo wa kufanya zaidi ili Tanzania iogopwe na isiwe njia wala duka la kufanya dawa za kulevya,” aliongeza.

Alielezea kuridhishwa kwake na mwelekeo uliochukuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan katika vita dhidi ya dawa za kulevya, na akabainisha kuwa mafanikio yameanza kuonekana kupitia kukamatwa kwa kiasi kikubwa cha dawa hizo.

Pia, Waziri Lukuvi amewahakikishia watumishi wa DCEA kuwa Serikali itaendelea kuwaunga mkono katika jitihada zao za kupambana na tatizo hili. Alionya kuwa Serikali haitasita kuchukua hatua dhidi ya wahalifu wa dawa za kulevya na itahakikisha kuwa Tanzania haifanywi kuwa lango la biashara hii haramu.

Mhe. Lukuvi akipokea maelezo kuhus Maabara ya DCEA kutoka kwa Kamishna wa Uchuguzi na Sayansi Jinai.

Mhe. Lukuvi akipokea maelezo kuhus Maabara ya DCEA kutoka kwa Kamishna wa Uchuguzi na Sayansi Jinai.

Mhe. Lukuvi akipokea maelezo kuhusu Kituo cha  Taarifa na Msaada kwa Simu cha DCEA.