Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Waziri Mkuu

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana Dawa za Kulevya

( DCEA )

Wadahiliwa Wapya Mwalimu Nyerere waelimishwa kuhusu Dawa za Kulevya

Imewekwa: 29 October, 2021
Wadahiliwa Wapya Mwalimu Nyerere waelimishwa kuhusu Dawa za Kulevya

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) tarehe 28 mwezi Oktoba 2021, imetoa elimu juu ya tatizo la dawa za kulevya katika Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kilichopo Kigamboni jijini Dar es Salaam. Lengo ni kuwasaidia wanachuo wa mwaka wa kwanza kujiepusha na matumizi ya dawa za kulevya na kutoshawishika kushiriki kwenye biashara ya dawa hizo.

Afisa Elimu wa Mamlaka wakati akitoa elimu amesema, wanafunzi wengi wa Vyuo hujiingiza kwenye matumizi ya dawa za kulevya kutokana na kufuata mikumbo, tamaa ya maisha mazuri na starehe. Amewasihi kuzingatia masomo na kufahamu kuwa, wako chuoni hapo kwa sababu maalum na wakati maalum.

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya imekuwa ikitoa elimu katika shule za Msingi na Sekondari, kamati mbalimbali, matamasha na matukio ya Kitaifa kama vile Sabasaba, Nanenane, Wiki ya UKIMWI Duniani, Wiki ya Vijana na Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru.


fBaadhi ya wanafunzi wakijadili ujumbe ulioko kwenye kipeperushio cha dawa za kulevya


fMmoja wa washiriki akiuliza swali baada ya wasilisho la mada juu ya dawa za kulevya


f