Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Waziri Mkuu

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana Dawa za Kulevya

( DCEA )

Tokomeza unyanyapaa kwa waraibu wanawake na wasichana

Imewekwa: 01 March, 2021
Tokomeza unyanyapaa kwa waraibu wanawake na wasichana

Leo ni siku ya kukomesha unyanyapaa Duniani (Zero Discrimination Day) ambayo huadhimishwa na Umoja wa Mataifa na Mashirika mengine Duniani kila ifikapo tarehe 01 Machi kila mwaka.

Ikiwa lengo la siku hii ni kuhamasisha USAWA katika jamii zetu hususani kwa makundi ambayo yamekuwa yakinyanyapaliwa kutokana na hali walizonazo au mambo tofauti waliyoyapitia, Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa Za Kulevya inaungana na juhudi zote zinazofanyika kupinga unyanyapa kwa waraibu wa dawa za kulevya tukiamini kwamba waraibu ni watu kama watu wengine hivyo wanastahili kuthaminiwa na jamii yote.

Ujumbe wa Mwaka 2021 kuhusu siku hii ni ‘Zero Discrimination Against Women and Girls’ . Katika jamii yetu wanawake na wasichana wameingia kwenye wimbi la matumizi ya dawa za kulevya kutokana na sababu mbalimbali ila wamekuwa na changamoto ya kujitokeza kupata huduma ili waachane na dawa hizo kutokana na unyanyapaa ulioko kwenye jamii. hivyo basi, katika siku ya leo Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na dawa za kulevya imetumia siku hii muhimu na waraibu kushiriki pamoja na waraibu wanawake na wasichana walioko jijini Dar es Salaam kujadili changamoto wanazokutana nazo.na namna ya kukabiliana nazo.

Aidha, Mamlaka inatoa wito kwa jamii kutokuwanyanyapaa wanawake na wasichana hawa pamoja na waathirika wote wa dawa za kulevya ili waweze kujitokeza kwa ajili ya kupata huduma za tiba.

.