Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Waziri Mkuu

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana Dawa za Kulevya

( DCEA )

Ofisa Usalama wa Posta na mwenzake wafikishwa Mahakamani.

Imewekwa: 04 October, 2019
Ofisa Usalama wa Posta na mwenzake wafikishwa Mahakamani.

Jamhuri imewafikisha mahakamani ofisa usalama awa Shiriksa la Posta Tanzania George Mwamgabe (44) na dereva Abraham Msimu (54) wakikabiliwa na mashtaka mawili ya kusafirisha dawa za kulevya.

Washtakiwa hao wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jana na kusomewa mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi MwandamiziAugustine Mmbando. Wakili wa Serikali, Adolf Lema, alidai Agosti 25 mwaka 2018 katika eneo la posta, Dar es Salaam washtakiwa hao kwa pamoja walisafirisha dawa za kulevya aina ya bangi gram 124.55.

Kosa la pili ni la kusafirisa dawa za kulevya aina Heroine Hydrochloride zenye uzito wa gramu 1.55 ambapo pia wanadaiwa walilitenda pia Agosti 25, 2018 katika jiji la Dar es Salaam.

Kwa pamoja washitakiwa hao wamekana makosa hayo na upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika. Washitakiwa hao wameomba wapatiwe dhamana ambapo mahakama imewapa masharti ya kuwa na wadhamini wawili watakaosaini bondi ya Sh. mil tano kila mmoja na mmoja wa wadhamini awe mtumishi wa serikali.

Washtakiwa hao wameshindwa kutimiza masharti ya dhamana, hivyo wamerudishwa rumande na kesi imeahirishwa hadi Oktoba 16, mwaka huu.