Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Waziri Mkuu

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana Dawa za Kulevya

( DCEA )

Mkakati wa kutokomeza watumiaji na wauza Dawa za Kulevya wasukwa

Imewekwa: 26 September, 2019
Mkakati wa kutokomeza watumiaji na wauza Dawa za Kulevya wasukwa

Kutokana na tatizo la matumizi ya Dawa za Kulevya kwa makundi tofauti katika jamii ndani nan je ya jiji la Dar es salaam, Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) kupitia divisheni ya Kinga na Tiba wameweka mkakati wa kupunguza matumizi ya Dawa za Kulevya kwa kutoa elimu ya athari za Dawa za Kulevya kwa makundi hayo.

Katika kutekeleza mkakati huo, Mamlaka imeanza programu ya uelimishaji kwa baadhi ya shule za sekondari na msingi jijini Dar es salaam. Utafiti unaonesha kuwa baadhi ya wanafunzi katika shule hizo ni wahanga wa matumizi na biashara ya dawa za kulevya.

wanafunzi wa shule ya sekondari Mgabe wakipata elimu

Lengo ni kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu sahihi juu ya biashara haramu ya dawa za kulevya, matumizi ya dawa za kulevya kama mirungi, bangi, cocaine, heroin na dawa tiba zenye asili ya kulevya; ikiwa ni pamoja na kujua athari zinazoletwa na matumizi ya dawa hizo. Pia kuwapa ushauri nasaha wale waliokwishaanza matumizi ya dawa hizo na kuathirika


.Mpaka sasa shule za sekondari zilizofikiwa ni Mugabe, Yusuph Makamba, Turiani, kigogo mapera na Manzese. Hata hivyo Mamlaka inaendelea na uelimishaji na imepanga kuzifikia shule nyingi, vyuo na makundi mbalimbali Tanzania nzima.fYusuph Makamba