Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Waziri Mkuu

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana Dawa za Kulevya

( DCEA )

Mamlaka yagawa vifaa tiba vya kujikinga na magonjwa ambukizi pamoja na taulo za kike kwa waathirika wa Dawa za Kulevya

Imewekwa: 30 September, 2020
Mamlaka yagawa vifaa tiba vya kujikinga na magonjwa ambukizi pamoja na taulo za kike kwa waathirika wa Dawa za Kulevya

Kamishna Jenerali wa Mamlaka wa Kudhibita na Kupambana na Dawa za Kulevya, James Wilbert Kaji,amekabidhi vifaa tiba vya kujikinga na magonjwa ambukizi pamoja na taulo za kike (Sanitary Pads) kwa waathirika wa dawa za kulevya, waliopo kweye vituo vya Methadone pamoja na nyumba za upataji nafuu (Sober House) nchini

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dae e salaam wakati wa kukabidhi vifaa hivyo Kamishna Jenerali Kajialisema,vifaa hivyo vimetolewa Mamlaka kwa kushirikiana na Umoja wa Nchi za Ulaya (EU) pamoja na Flaviana Matata Foundation. Ikiwa ni moja ya majukumu ya Mamlaka kushughulikia huduma za utengamao na tiba kwa waathirika wa dawa hizo.

Alisema, Umoja wa Nchi za Ulaya kupitia Mradi wa EU-ACT wametoa mashine 12 za kunawia mikono pamoja na sabuni zake kwa vituo vya Methadone nchini. Ambapo Mwanamitindo Mtanzania Flaviana Matata kupitia taasisi ya Flaviana Foundation wametoa taulo za kike (Sanitary Pads) kwa wanawake wanao pata huduma za utengamao kutokana na matumizi ya dawa za kulevya waliopo kwenye nyumba za upataji nafuu (Sober House).

Akikabidhi vifaa hivyo Kamishna Jenerali Kaji aliishukuru Serikali ya Awamu ya Tano ikiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa kutambua athari ambazo husababishwa na tatizo la dawa za kulevya hasa kijamii, kiafya, kisiasa, kiuchumi na kidiplomasia ilianzisha Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya rasmi mnamo mwezi Februari mwaka 2017.

Kamishna Jenerali Kaji pia aliwashukuru wadau wote wa maendeleo ambao wamekuwa mstari wa mbele katika kushirikiana na Mamlaka katika jitihada mbalimbali za kupambana na tatizo la dawa za kulevya. Ambapo kipekee, limshukuruFlaviana Matata ambaye ameonesha uzalendo wa kipekee kwa kuwasaidia kinamama ambao wameathirika na matumizi ya dawa za kulevya.

“Naomba wadau wengine wazidi kujitokeza zaidi kama alivyofanya Flaviana Matata na Umoja wa Nchi za Ulaya katika kuendeleza ushirikiano kwa kuwa tatizo hili ni suala mtambuka na linahitaji ushirikiano kutoka katika Wizara mbalimbali na Taasisi za Serikali, Kiraia, Kimataifa na jamii yote ya watanzania kwa ujumla” alisema Kamishna Jenerali Kaji.

Aliendelea kusema kuwa, mpaka sasa kuna jumla ya vituo tisa (9) vya Methadone Nchini vilivyopo kwenye Hospitali ya taifa yaMuhimbili, Hospitali za Temeke, Mwananyamala, Mbeya, Mwanza, Tanga, Dodoma na Bagamoyo ambavyo vinatoa tiba ya uraibu wa dawa za kulevya na takribani waathirika 8000 wanapata huduma hizo kila siku. Na kwa upande wa nyumba za upataji nafuu (Sober houses), kuna jumla ya nyumba ishirini na tisa (29), kati ya hizo ni nyumba tatu (3) tu zinazohudumia wanawake. Nyumba zinazohudumia wanawake zipo katika mikoa ya Kilimanjaro (Hai), Pwani (Bagamoyo) na Dar es salaam (Kigamboni) na zina jumla ya wanawake 35.

Mwisho aliwashukuru waandishi wa habari kwa kuwa mstari wa mbele katika kuhabarisha wananchi, ambapo alisema hii ni ishara tosha kwamba wanaunga mkono vita dhidi ya tatizo la dawa za kulevya nchini.