Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Waziri Mkuu

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana Dawa za Kulevya

( DCEA )

Mahakama ya Rufaa Yatupilia mbali Rufaa ya Khamis Said Bakari

Imewekwa: 01 June, 2020
Mahakama ya Rufaa Yatupilia mbali Rufaa ya Khamis Said Bakari

Mahakama ya Rufani iliyokaa jijini Dar es Salaam tarehe 13/05/2020 imetupilia mbali Rufaa namba.359 ya mwaka 2017 iliyokatwa na Khamis Said Bakari dhidi ya Jamhuri.

Khamis alihukumiwa na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam tarehe 23/8/2017 kutumikia kifungo cha miaka 20 na kulipa faini ya shilingi 130,172,400/= baada ya kuthibitika kukamatwa na gramu 964.24 za heroin, ambapo alihukumiwa kwa kukiuka kifungu cha 16(1) (b) cha Sheria ya Kudhibiti Biashara Haramu ya Dawa za Kulevya na. 9 ya mwaka 1995.

Mahakama ya Rufani ilisikiliza rufani hiyo tarehe 13/05/2020 na kutoa hukumu ya rufaa husika tarehe 29/05/2020 kwa Jamhuri kushinda rufaa hiyo.

Hivyo khamis ataendelea kutumikia kifungo cha miaka 20 pamoja na adhabu ya faini kama ilivyotolewa na Mahakama Kuu.