Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Waziri Mkuu

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana Dawa za Kulevya

( DCEA )

Mahakama yamhukumu kwenda jela miaka 30 mtuhumiwa wa dawa za kulevya

Imewekwa: 15 April, 2020
Mahakama yamhukumu kwenda jela miaka 30 mtuhumiwa wa dawa za kulevya

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemhukumu kwenda jela miaka thelathini (30) Shaban Ramadhani Abdala @Kindamba (27) kwa kosa la kukutwa na dawa za kulevya aina ya Heroin gramu 50. 83.

Hukumu hiyo ilisomwa tarehe 10 Machi mwaka huu na Hakimu Victoria Mwaikambo baada ya ushahidi uliotolewa mahakamani hapo kuthibitisha pasipo shaka yoyote kwamba Bw. Kindamba anajihusisha na biashara ya dawa za kulevya.

Bw. Kindamba ametiwa hatiani na Kifungu cha 15 (1) (a) na (2) cha Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Na.5 ya Mwaka 2015 na aya ya 23 ya Jedwari la kwanza la kifungu cha 57 (1) cha Sheria ya Uhujumu Uchumi Sura ya 200.

Shabani alikamatwa na maofisa wa Mamlaka tarehe 1 Mei 2018 nyumbani kwake Kigamboni eneo la Kabaoni Mjimwema baada Mamlaka kubaini anajihusisha na biashara hiyo haramu na kufanikiwa kumkuta na kiasi hicho cha dawa.