Kamishna jenerali Lyimo kuanza na vijiwe vyote, vita dhidi ya dawa za kulevya
Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Aretas James Lyimo ametaja malengo yake katika kupambnana na dawa za kulevya nchini. Kamishna Lyimo ameyasema hayo mbele ya waandishi wa habari tarehe 1 aprili, 2023 mkoani Mtwara kwenye tukio la uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa ambapo Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya imeshiriki kutoa elimu kwa jamii juu ya madhara yamatumizi na biashara ya dawa za kulevya.
“Mimi kama kamishna mpya wa Mamlaka hii, malengo yangu niliyoingia nayo ni kuhakikisha tunadhibiti kabisa uingizaji na usambazaji wa dawa za kulevya nchini. Kwahiyo nitoe wito kwa watumiaji wa dawa za kulevya kuacha kutumia dawa hizo lakini pia wale wauzaji na wasambazaji wa dawa hizi kuacha kabisa biashra hiyo kwani tunafanya operesheni kabambe nchi nzima, na tutahakikisha vijiwe vyote vya wauzaji , na watumiaji wa dawa za kulevya vinasambaratishwa” Amesema kamishna jenerali Lyimo.
“Tutafafanya operesheni nchi nzima na tutawakamata wanaofanya biashara ya dawa kulevya. Lakini pia tutafanya operesheni kijiji kwa kijiji mikoa yote kuhakikisha kwamba wale wote wanaolima bangi na mirungi tunawakamata na kuteketeza mashamba yao. Kwa hiyo nitoe wito kwa wananchi, mashirika ya dini na serikali kwa ujumla kuhakikisha kwamba tunatoa taarifa wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya ili kuweza kufanikisha operesheni mbalimbalikatika kudhibiti dawa za kulevya”amefafanu Kamishna Jenerali Lyimo.
Aidha, ametoa wito kwa jamii kutambua kuwa ushirikiano wao utaiwezesha nchi kuwa salama na huru bila dawa za kulevya, kwani dawa za kulevya zina madhara makubwa sana kijamii, kiafaya, kimazingira na kiuchumi kwani zinapotezaq huchangia kupoteza nguvu kazi ya Taifa.
Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa zimezinduliwa na waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tainzania Mhe. Kassim MajaliwaMajaliwa mkoani Mtwara katika uwanja wa Nangwanda sijaona, ambapo Mamlaka ya Kudhibi na Kupambana na Dawa za Kulevya imeshiriki katika utoaji wa elimu kwani ina ujumbe wa kudumu katika mbio hizo.
Maofisa wa Mamlaka wakitoa elimu ya dawa za kulevya kwenye maonesho ya uzinduzi wa Mbio za Mwenge katika viwanja vya Sabasaba mkoani Mtwara
“Sisi ni sehemu ya Mwenge, na kwa sababu mwenge unatembea nchi nzima kwa ajili ya kukemea maovu na kuhakikisha kuwa maovu yanaondoka kwenye jamii; dawa za kulevya ni moja ya maovu yanayokemewa na mwenge hivyo tuko hapa kuitaka jamii iachane na matumizi ya dawa za kulevya na mwisho wa siku kuhakikisha tunakuwa na Tanzania isiyojihusisha na biashara wala matumizi ya dawa za kulevya” amesema Kamishana Jenerali Aretasi Lyimo aliyeteuliwa mwishoni mwa Mwezi Machi, 2023 na Rais wa Jamhauri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassani Kuiongoza Mamlaka na Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya.
Kamishna Jenerali Aretas Lyimo akizungumza na waandishi wa habari