Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Waziri Mkuu

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana Dawa za Kulevya

( DCEA )

Kamishna Jenerali Kusaya Afanya Mazungumzo na Katibu Mkuu UNODC

Imewekwa: 21 March, 2022
Kamishna Jenerali Kusaya Afanya Mazungumzo na Katibu Mkuu UNODC

Kamishna jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Gerald Musabila Kusaya na ujumbe kutoka Tanzania amefanya mazungumzo na katibu mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa Linaloshughulikia Dawa za Kulevya na Uhalifu wa Kupangwa (UNODC) Bi. Ghada Fathi Walli kujadili namna bora ya kuimarisha mapambano dhidi ya dawa za kulevya Nchini Tanzania na Kimataifa.

Mazungumzo hayo yamefanyika mara baada ya kuhitimishwa kwa Mkutano wa 65 wa Kamisheni ya Kimataifa ya Kupambana na Dawa za Kulevya uliofanyika tarehe 14 hadi 18 Machi, 2022 jijini Vienna – Austria ukiwa na lengo la kuangalia namna bora ya kupambana na dawa za kulevya Pamoja na kukabiliana na changamoto mbalimbali katika udhibiti wa dawa hizo duniani.



h