Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Waziri Mkuu

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana Dawa za Kulevya

( DCEA )

Kamishna Jenerali DCEA Atembelea Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali

Imewekwa: 06 September, 2021
Kamishna Jenerali DCEA Atembelea Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali

Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Gerald Musabila Kusaya ametembelea Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA), Makao Makuu kuweza kuona namna shughuli za uchunguzi wa kimaabara wa sampuli za dawa za kulevya unavyofanyika. pia ameipongeza Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa kazi kubwa wanayoifanya hasa kwenye uchunguzi wa kimaabara wa sampuli za dawa za kulevya ambapo umekuwa ukifanyika kwa haraka na uhakika kutokana na kuwa na Wataalam wabobezi na mitambo ya kisasa inayotumika katika uchunguzi kwenye maabara.

Katika ziara hiyo Kamishna Jenerali Kusaya aliweza kutembelea maabara za Maabara ya Sayansi Jinai Kemia, Toksikolojia na Maabara ya Mitambo.

wKamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Gerald Kusaya (kushoto) akisalimiana na Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (Kulia )mara baada ya kuwasili Mamlaka, Makao Makuu tarehe 30 Agosti, 2021.


Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (katikati) akifafanua jambo alipokuwa akizungumza na Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya ,Gerald Kusaya (wa tatu kulia), pamoja na Kamishna wa Uchunguzi wa Sayansi Jinai, Bertha Mamuya (wa pili kulia) na Kamishna wa Oparesheni, Luteni Kanali Frederick Millanzi (kulia). Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kutoka DCEA, Florence Khambi, Mkurugenzi wa Huduma za Udhibiti, Daniel Ndiyo na Mkurugenzi wa Huduma za Sayansi Jinai, David Elias


Meneja wa Maabara ya Toksikolojia, Kagera Ng’weshemi (kushoto) akitoa ufafanuzi juu ya Mtambo wa Kisasa wa LC-MS/MS unavyochunguza Sampuli mbalimbali kwa wakati mmoja ikiwemo za Dawa za Kulevya.