Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Waziri Mkuu

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana Dawa za Kulevya

( DCEA )

Kaimu Kamishna Jenerali Azindua Kituo cha Kutoa Elimu ya Dawa za Kulevya.

Imewekwa: 20 November, 2019
Kaimu Kamishna Jenerali  Azindua Kituo cha Kutoa Elimu ya Dawa za Kulevya.

Kaimu kamishna jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Bw. James Kaji leo amezindua kituo cha utoaji elimu ya dawa za kulevya katika eneo la soko la samaki la feri jijini Dar es Salaam.

Katika uzinduzi huo kamishna Kaji ameziomba taasisi na jamii kushirikiana katika kutoa elimu ya dawa za kulevya na kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Mhe. Rais Magufuli katika kutengeneza taifa lililo imara. Pia ametoa wito kwa wananchi kuendelea kuwafichua waharifu wa dawa za kulevya huku akimpongeza Pili Misana mwanzilishi wa sober house Tanzania bara kwa kazi nzuri aliyoifanya.

Akizungumzia lengo la ufunguzi wa kituo hicho, mkurugenzi wa Pili Misana Foundation ambae pia ni mwanzilishi wa Back to Life Sober House amesema lengo ni kutoa elimu ya dawa za kulevya bure kwa watu wote na kuhakikisha tunakuwa na taifa lisilo na watumiaji wa dawa za kulevya hivyo anawakaribisha watu wote kufika katika banda na kujifunza.

Pilli Missana Foundation ni Taasisi inayojihusisha na kuwasaidia vijana wanaojihusisha na matumizi ya dawa za kulevya. Taasisi hii hutoa elimu ya namna ambayo mtu anaweza kuachana na dawa za kulevya. Vijana wanajengwa kiimani, kielimu na kimaadili pia.

Taasisi hii yenye makazi yake kigamboni jijini Dar es Salaam imefanikiwa kuwajenga upya vijana waliookuwa wategemezi wa dawa za kulevya na kuwa watu wema wanaolitumiki taifa.