(DCEA)
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) kwa kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (NPS) wameendesha mafunzo kwa wapelelezi na waendesha mashtaka wa serikalijuu ya upelelezi na uendeshaji wa mashauri ya dawa za kulevya, leo tarehe 31 Julai, 2023 mkoani Morogoro.
Kamishna wa Huduma za Sheria wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Bi. Veronica Matikila amesema, mafunzo haya yanafanyika kufuatia maelekezo yaliyotolewa na Baraza la Taifa la Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya kwa DCEA na NPS kuhakikisha wanafanya mafunzo endelevu kwa maafisa wanaopeleleza na wanaoendesha mashauri ya dawa za kulevya ili kukabiliana na changamoto za kiutendaji na ikiwa ni pamoja na kubadilishana uzoefu juu ya mashauri ya dawa za kulevya .
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya
S.L.P 80327
8 Barabara ya Kivukoni Front, 11486 Dar es salaam
Dar es Salaam
Simu: +255 22 211 3754/57
Nukushi: +255 22 211 3752
Barua pepe: cg@dcea.go.tz
© 2023 Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya. Haki zote zimehifadhiwa..
Imesanifiwa, Imetengenezwa, na Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) na Inaendeshwa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya