Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Waziri Mkuu

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana Dawa za Kulevya

( DCEA )

Elimu ya Dawa za Kulevya Shuleni Kujenga Taifa Imara

Imewekwa: 29 October, 2019
Elimu ya Dawa za Kulevya Shuleni Kujenga Taifa Imara

Tatizo la matumizi ya Dawa za Kulevya limeendelea kutamalaki katika maeneo mbalimbali nchini. Licha ya jitihada zinazofanywa na serikali na taasisi nyingine zisizo za kiserikali kupambana na tatizo hili, bado matumizi ya biashara ya dawa za kulevya yameendelea kuwepo na kushika kasi huku wahanga wakubwa wakiwa ni vijana. Hii ndio sababu Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za kulevya (DCEA) imeamua kuwekeza katika kutoa elimu ya dawa za kulevya kwa wanafunzi.

Katika kudhibiti matumizi na biashara ya dawa za kulevya, Mamlaka imeendelea kutembelea shule mbalimbali za sekondari katika viunga vya jiji la Dar es salaam; na mwishoni mwa wiki maofisa wa Mamlaka walitembelea shule za sekondari Chalambe na Mbande zilizo wilaya ya Temeke jijii Dar es Salaam.

Mkuu wa shuke ya sekondari Mbande Bw. Godfrey Nchimbi amesema tatizo la Bangi limekithiri shuleni hapo. Baadhi ya wanafunzi wanauza na wengine wanatumia.Waathirika wakubwa ni wanafunzi wa kidato cha kwanza na cha pili na wengi wao hulazimika kuacha shule wanapofika kidato cha tatu kutokana na utoro sugu hivyo kubanwa na sheria za shule na kufukuzwa.

m

"moja ya sababu ya wanafunzi kujihusisha na dawa za kulevya ni msumkumo wa kimazingira. Shule hii iko katikati ya makazi ya watu na wengi wa wakazi hao hujihusisha na biashara hiyo haramu huku wakiwatumia wanafunzi kuuza. Kuna wakati hatufundishi tunaingia katika kazi ya kuwasaka huko wanakotokomea. Unawasaka mwisho wa siku unachoka unaacha. Lakini tukiacha pia wanaendelea kuwapenyezea wengine ambao hawajihusishi. Majirani hawatupi sapoti yoyote maana ndio biashara yao. Pia shule za kata zimechangia kwa sababu wanafunzi kutoka shule moja na kwenye mazingira mamoja wanahamishiwa kwenye shule moja ya sekondari hivyo kunakuwa na muendelezo wa tabia hatarishi ".

Nae mkuu wa shule yya sekondari Chalambe Bw. Shukuru Lucas Nkokelo akizungumzia tatizo la dawa za kulevya shuleni kwake amesema, "Haya mafunzo tunayahitaji sana shuleni kwetu maana yanasaidia katika kurekebisha tabia. Hapa shuleni kuna wanafunzi wanauza na wengine ni wavuta bangi. Kuna binti wa kidato cha pili alikamatwa na kete 52 za bangi akiwa amejificha nazo chooni hivi karibuni ".

Kwa ujumla mazingira ya shule zote mbili sio rafiki sana kwani yameingiliana sana na maeneo ya makazi na hakuna uzio. Hata hivyo maafisa kutoka DCEA wamefanikiwa kutoa elimu ya dawa ya kulevya shuleni hapo huku wakishuhudia vitendo vingi vya utovu wa nidhamu na baadhi ya wanafunzi walikuwa na vitambaa vilivyochorwa mmea wa bangi na kuvionyesha wakati wa kipindi cha uelimishaji.

m

m

m