Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Waziri Mkuu

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana Dawa za Kulevya

( DCEA )

DCEA Yateketeza zaidi ya Kilo 190 za Heroin na Cocaine Jijini Dar es Salaam

Imewekwa: 11 October, 2019
DCEA Yateketeza zaidi ya Kilo 190 za Heroin na Cocaine Jijini Dar es Salaam

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imefanya uteketezaji wa zaidi ya kilo gramu 190 za dawa za kulevya jijini Dar es Salaam. Dawa hizo ni Heroin kilo gramu 120.91 au (120,919.88 gramu) na Cocaine kilo 70.96 (70,967.86 gramu).Uteketezaji huo umefanyika katika kiwanda cha Saruji cha Wazo hill mbele ya Jaji Lilian Mashaka, Mkurugenzi wa mashtaka wa Tanzania (DPP) Ndg. Biswalo Mganga; Wawakilishi wa Baraza la Taifa la Mazingira , Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Jeshi la Polisi, Idara ya Usalama wa Taifa, Makamishna kutoka DCEA na Waandishi wa Habari.DAWA

Akizugumza katika uteketezaji huo, Kaimu Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Bw. James Wilbert Kaji amesema uteketezaji huo umefanyika kwa dawa ambazo kesi zake zimekwisha hukumiwa. “katika mzigo wote ulioteketezwa leo ni jumla ya kesi 35 zilizohukumiwa katika mahakama mbalimbali, na katika kilo 120 za Heroin kuna kilo 63.155 ambazo zilikamatwa Mtwara na kesi yake iliamriwa tarehe 27/09/2019 zikiwahusisha Mwinyi Kitwana Rajabu na Ally Hamdan Hamad "

DAWA

Aidha, Kamishna Kaji amewaomba wananchi kutoa ushirikiano kwa Mamlaka ili kuwafichua wanaojihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya. Pia ametoa onyo kwa wasambzaji, watumiaji na wasafirishaji wa dawa hizi haramu kuachana na dawa hizo na badala yake kuunga mkono jitihada za mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli katika kujenga nchi na kutengeneza Taifa lenye watu wenye afya ya akili ambao wanaweza kulitumikia taifa lao.

Akizungumzia sheria ya uteketezaji kwa mujibu wa Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Kamishna wa Huduma za Sheria wa DCEA Bw. Edwin Kakolaki amesema“ili dawa za kulevya ziteketezwe lazima kuwe na amri ya Mahakama iliyosikiliza kesi na kumalizika au ambapo kesi hiyo ipo. Pia uteketezaji wa dawa za kulevya hufanyika kwa utaratibu maalumu ili kuepuka uharibifu wa mazingira na madhara ya kiafya”

DAWA

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Mamlaka ya Kudhibiti na kupambana na Dawa za Kulevya, uteketezaji huu ni wa kwanza kwa mwaka huu, ambapo uteketezaji kama huu ulifanyika mwaka 2015 katika kiwanda hicho hicho na ulihusisha uteketezaji wa dawa za kulevya aina mbalimbali.

Nae Mkurugenzi wa Mashtaka nchini amewashukuru watendaji na wananchi wote waliofanikisha watuhumiwa kukamatwa na kutiwa hatiani. Pia amesisitiza kuwa dawa zilizoteketezwa ni za mikoa miwili tu yaani Mtwara na Dar es Salaam ambazo kesi zake zimesikilizwa katika Mahakama kuu, na Mahakama Kuu Kitengo cha Rushwa na Uhujumu Uchumi. “katika kesi hizi kulikuwa na washtakiwa 39;kati ya hao washtakiwa 26 wamehukumiwa kifungo cha miaka 20 au kifungo cha maisha, washtakiwa wanne walifariki kabla kesi zao hazijakamilika na mshtakiwa mmoja pekee ndiye aliyeachiwa huru”.

Pia DPP amewaomba waandishi wa habari kuwaelimisha wananchi juu ya madhara ya kujihusisha na biashara haramu

DAWA