Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Waziri Mkuu

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana Dawa za Kulevya

( DCEA )

DCEA Yashiriki Maadhimisho Wiki ya Vijana Kitaifa

Imewekwa: 11 October, 2022
DCEA Yashiriki Maadhimisho Wiki ya Vijana Kitaifa

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) inashiriki Maadhimisho ya Wiki ya Vijana yanayofanyika kitaifa mkoani Kagera katika viwanja vya Gymkhana Bukoba Mjini. Kauli mbiu ya mwaka huu inasema “Kila Mmoja Anahusika Katika Kujenga Uchumi Imara na Ustawi wa Maendelo Endelevu.

Maadhimisho hayo yaliyoanza tarehe 08 hadi 14 Oktoba, 2022 yatafunguliwa rasmi na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa majaliwa (Mb) siku ya Jumatano tarehe 12 Oktoba 2022.

Aidha, kupitia banda la Mamlaka lilipo katika viwanja hivyo, huduma mbalimbali zinatolewa kama vile, elimu kuhusiana na madhara ya matumizi na biashara ya dawa za kulevya, kemikali bashirifu na udhibiti wake, na Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya.

Pia, wananchi wa mkoa wa Kagera wanapata fursa ya kupata maelezo kuhusu huduma mbalimbali za tiba na huduma za utengamao kwa waraibu wa dawa za kulevya zinazotolewa Nchini ikiwa ni pamoja na ushauri kwa waraibu wa dawa hizo; na wananchi watapata fursa ya kuziona dawa za kulevya katika uhalisia wake.

Kamishna msaidizi wa Tiba na Huduma za Utengamao wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Dkt. Cassian Nyandindi amewasihi wananchi kuendelea kutembelea banda la Mamlaka ili wapate elimu sahihi kuhusu tatizo la dawa za kulevya na waitumie elimu watakayoipata kuwaelimisha wengine kwani mapambano dhidi ya tatizo la dawa za kulevya yanahitaji ushiriki wa kila mmoja.


u