Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Waziri Mkuu

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana Dawa za Kulevya

( DCEA )

DCEA yaibuka mshindi wa kwanza katika kundi la Wizara na Idara za Serikali tuzo za NBAA

Imewekwa: 05 February, 2021
DCEA yaibuka mshindi wa kwanza katika kundi la Wizara na Idara za Serikali tuzo za NBAA

MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imekuwa mshindi wa kwanza wa umahiri katika uandaaji wa Taarifa za Fedha ya Mwaka 2019 (Best Presented Financial Statements for the Year 2019 Awards) katika kundi la Wizara na Idara za Serikali. Tuzo hizo zinatolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) zimefanyika jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kupokea tuzo hiyo, muwakilishi wa kamishna jenerali wa Mamlaka amesema, kupokea tuzo hii kwa mara tatu mfululizo inaonyesha wazi namna gani ambavyo matumizi ya fedha na uwasilishaji wa hesabu umekaa vizuri. “tuko mbele katika kupambana na dawa za kulevya lakini tuko vizuri pia katika masuala ya matumizi na uwasilishaji wa fedha za serikali ’’amesema.

Naye Mhasibu mkuu wa DCEA CPA Stephen Dalasia amesema kushinda kwa nafasi hiyo ni heshima kwa Taasisi na kunaonesha wahasibu wanajua kazi wanayofanya na wanazingatia viwango.

‘‘Kupata kwa tuzo hii kwa mara nyingine kuna maana kubwa sana kwa taasisi yetu sambamba na wahasibu waliopo kwenye kitengo cha fedha, hivyo tunaahidi kuendelea kuwa katika viwango bora kila siku kwani kupata kwa tuzo hii kumeleta chachu kubwa kwenye taasisi na kitengo kwa ujumla’’amesema Dalasia.

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya imekuwa ikishiriki katika mashindano haya tangu mwaka 2014/2015 na mwaka huu imeendelea kuwa mshindi wa kwanza kwa mara ya tatu mfulizo.