DCEA Yakamata Mtandao wa Kitaifa wa Dawa za Kulevya
DCEA Yakamata Mtandao wa Kitaifa wa Dawa za Kulevya
09 November, 2026
Pakua
Tarehe 6 Novemba 2026, eneo la Mwenge, jijini Dar es Salaam, Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) ilifanya operesheni na kufanikiwa kukamata jumla ya paketi 299 za dawa za kulevya, zikiwemo paketi 24 za heroin na paketi 275 za methamphetamine. Dawa hizo zilikamatwa zikiwa zimefichwa ndani ya magari mawili aina ya Ford Ranger yenye namba za usajili T.950 ERA na T.417 EJZ, ambayo pia yanashikiliwa kutokana na kuhusishwa na uhalifu huo. watuhumiwa wanne (4) walikamatwa katika operesheni hiyo